Jux Kuyaanika Maisha ya Vee Kwenye Zaidi. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Jux Kuyaanika Maisha ya Vee Kwenye Zaidi.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’ hivi karibuni ameachia video yake mpya ya Ngoma ya Zaidi ambayo hadi gazeti hili linakwenda mtamboni kwa upande wa Tanzania ilikuwa ni namba tano kwenye ngoma zinazotrendi.


Simulizi ya video hiyo ni namna ambavyo Jux alikuwa amezama kwenye penzi zito la mwanadada ambaye alikuwa anasomea sheria na anakwenda mtaani kumtafuta alikomuona kwa mara ya kwanza.


Ukiicheki video hii, Jux ni kama ameweka maisha ya mpenzi wake, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ambaye naye ni mwanasheria wa ngazi ya digrii aliyesomea nchini Kenya kwenye Chuo cha Catholic University of Eastern Africa.


Akizungumzua juu ya hilo, Jux alisema: “Wakati ninaandaa namna video itakavyokuwa sikuwaza kuhusu hilo, lakini baadaye ndiye (Vee Money) alifahamu kwamba kwa namna moja au nyingine video hiyo inaendana na ukweli.”


The post Jux Kuyaanika Maisha ya Vee Kwenye Zaidi. appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More