JWTZ YAMTAKA ALIYELALAMIKIA HUDUMA HOSPITALI YA LUGALO AJITOKEZE KUBAINI UKWELI VINGINEVYO WATAMSAKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JWTZ YAMTAKA ALIYELALAMIKIA HUDUMA HOSPITALI YA LUGALO AJITOKEZE KUBAINI UKWELI VINGINEVYO WATAMSAKA

Na Luteni  Selemani SemunyuJeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limekanusha taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko juu matibabu  ya mtoto anayedaiwa kuvunjika na kupatiwa  huduma  katika Hospitali kuu ya jeshi ya Lugalo.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo  Jijini  Dar es Salaam msemaji mkuu wa Jeshi Kanali Ramadhani Dogoli alimtaka aliyejinasibisha kama mlalamikaji kuwasilisha malalamiko yake kama yana ukweli ili hatua zichukuliwe kwa wahusika.
“ Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ linamtaka malalamikaji alete taarifa kwenye uongozi ili kama matukio hayo yametokea tuweze kuchukua hatua kwa wahusika” Alisema kanali Dogoli.
 Aliongeza kuwa iwapo aliyedai kulalamika atashindwa kufanya hivyo jeshi litaaamini kuwa mlalamikaji alikusudia kuichafua hospitali yetu kwa maslahi binafsi  na kwa sababu hiyo tutamtafuta haraka na kumchukulia hatua zinazomstahili.
Msemaji huyo wa JWTZ Mnamo Julai 10 mwaka huu ilisambaa habari ikilalamika huduma z... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More