KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Charles Kabeho akiongea na mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Njwayo ,wakati akikagua wodi ya watoto ikiwa ni sehemu ya majengo ya mradi wa kituo cha afya cha Ikwiriri ,Rufiji, mkoa wa Pwani.
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.
KIONGOZI wa mbio za mwenge mwaka huu, Charles Kabeho ,amekataa kuzindua mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani.
Hali hiyo imezua sintofahamu mara baada ya kusomwa ripoti ya matumizi ya fedha ambazo hazijaeleweka zimetumikaje huku serikali ikiwa imechangia kiasi cha sh.milioni 400.
Aidha kwa mujibu wa taarifa ya wilaya imedaiwa wananchi wamechangia milioni tatu wakati taarifa ya mkoa inaonyesha ilichangia milioni moja.Akizungumza kwenye kituo hicho cha afya, Kabeho alishtushwa na kuhoji kutokea kwa hali hiyo.
Alimtaka mkuu wa wilaya atoe kauli yake na kukataa kuuzindua mradi mpaka watakapotoa taarifa ya uhakika.Kabeho aliasa halmashauri na wilaya mbalimbali ,kusimamia miradi ya maendeleo ili iendane na thama... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More