KABWILI AWAFUATA NGORONGORO HEROES LEO KWA MCHEZO WA MARUDIANO NA MALI JUMAPILI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KABWILI AWAFUATA NGORONGORO HEROES LEO KWA MCHEZO WA MARUDIANO NA MALI JUMAPILI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIPA Ramadhani Awam Kabwili anaondoka leo Dar es Salaam kuifuata timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Mali Raundi ya pili ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika mwakani nchini Niger.
Kabwili hakuwepo kwenye msafara wa Ngorongoro Heroes ulioondoka Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kwa sababu alikuwa na klabu yake, Yanga SC iliyokuwa inamenyana na Rayon Sport ya Rwanda katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.
Na baada ya mchezo huo ambao chipukizi huyo alikuwa benchi akimtazama Mcameroon Youthe Rostand anavyookoa, Kabwili anawafuata wenzake leo kwenda kuipigania bendera ya nchi yake.
Ramadhani Kabwili anaondoka leo Dar es Salaam kuifuata Ngorongoro Heroes kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Mali Jumapili

Tanzania ilijiweka kwenye mazingira magumu ya kusonga mbele katika mbio za Niger 2019 baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mali kwenye mchezo ... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More