KADI ZA BENKI TU KUTUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA YANGA JUMAPILI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KADI ZA BENKI TU KUTUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA YANGA JUMAPILI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
UCHAGUZI mdogo wa klabu ya Yanga utafanyika kwenye Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay mjini Jumapili ya Januari 13, mwaka huu huku wanachamaa wa kadi za benki tu zilizohakikiwa wakiruhusiwa kuingia.
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo imesema kwamba kadi zitakazotumika katika Uchaguzi ni kadi za Kitabu na kadi za Benki zilizohakikiwa.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo imesema kwamba Kampeni za kuelekea Uchaguzi huo zimefunguliwa rasmi leo.
Akitangaza kufunguliwa kwa kampeni hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Malangwe Mchungahela amewataka wagombea kufanya kampeni kwa amani bila kumchafua mwingine.

Kama hamna kadi za benki msijisumbue kwenda kwenye uchaguzi Jumapili

Mchungahela ameongeza kuwa kila mgombea anaruhusiwa kujinadi kokote ikiwemo katika tawi lolote la Young Africans.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Young Africans ambaye pia ni Msaidizi wa Kaimu Mwenyekiti Siz... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More