Kaduguda afunguka kuhusu misimamo yake ‘Mimi siachi mwanamke ila ananiacha yeye, kwa nini uache raha ?’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kaduguda afunguka kuhusu misimamo yake ‘Mimi siachi mwanamke ila ananiacha yeye, kwa nini uache raha ?’

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT (sasa TFF) na klabu ya Simba, Mwina Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ amesema kuwa misimamo aliyowahi kuwa nayo katika maisha yake ya uongozi wa soka ndiyo aliyonayo hadi sasa kwenye maisha ya kawaida nyumbani.Kaduguda ameyasema hayo wakati wa mahojiano yake na Azam tv kupitia kipindi cha Nyundo ya Baruan Muhuza kinachoruka kila siku ya Alhamisi baada ya kuulizwa kuhusiana na watu namna wanavyo mchukulia kama mtu mtata ndipo akasema kuwa yeye ni mtu mwenye misimamo katika maisha.


”Mimi nina misimamo hata katika maisha yangu ya kawaida ya nyumbani kwangu wake zangu wanajua, mimi mke wangu akitaka kwenda kwa mwanaume mwingine sitaki anibabaishe anizungushe ana niambia moja kwa moja nimekuchoka nimechoka kuishi na wewe basi tunaachana anaondoka zake kwa sababu yeye kazaliwa kwao na mimi nimezaliwa kwetu,” amesema Mwina Kaduguda.


Kaduguda ameongeza ”Mimi siachi mwanamke, ila mwanamke ananiacha yeye sina matatizo kwa sababu mwanamke hapewi talaka. Tal... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More