KAGERE AIPELEKA SIMBA SC FAINALI KOMBE LA KAGAME…ITAKUTANA NA AZAM IJUMAA TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAGERE AIPELEKA SIMBA SC FAINALI KOMBE LA KAGAME…ITAKUTANA NA AZAM IJUMAA TAIFA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere limetosha kuipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba SC inakwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame na itakutana na Azam FC katika fainali Ijumaa hapa hapa Uwanja wa Taifa.
Kagere aliyesajiliwa mwezi uliopita kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa ndani ya boksi baada ya kupokea pasi mshambuliaji Mghana, Nicholas Gyan anayetumika kama beki kwa sasa.
Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akimuacha chini beki wa JKU leo Uwanja wa Taifa
Meddie Kagere akinyoosha mkono juu baada ya kuifungia Simba SC bao pekee leo

Pamoja na ushindi huo, Simba SC ilipata wakati mgumu kwa vijana wa Jesho la Kujenga Uchumi (JKU) waliokuwa wakiongozwa vizuri na kiungo hodari, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Ikumbukwe katika Nusu Fainali ... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More