KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.KAIMU Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.
Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Lizy Kiwia mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imedaiwa, Oktoba 25, 2012  huko katika ofisi kuu za TPA zilizopo, Temeke mshtakiwa huyo  wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722A kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. 
Akidai kuwa, garama ya  semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. 47,935,140 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.
Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa huyo wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722B kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. Ak... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More