KAIMU MTENDAJI KATA YA KENYAMANYORI ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UPOTEVU WA FEDHA, MIFUKO YA SARUJI 39 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAIMU MTENDAJI KATA YA KENYAMANYORI ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UPOTEVU WA FEDHA, MIFUKO YA SARUJI 39

Na Frankius Cleophace,Tarime
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara Elias Ntiruhungwa amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kenyamanyori Laurent Marwa kwa upotevu wa fedha za Serikali pamoja na mifuko 39 ya saruji ambayo ilipaswa kujenga vyumba viwili katika Shule ya Sekondari Kenyamanyori.
Akizungumza leo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa Kaimu huyo alienda kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkende na kusaini na kisha kukabidhiwa mifuko ya saruji huku akisubiliwa na wananchi waendelee na ujenzi katika Shule ya Sekondari Kenyamonyori.
Amefafanua lakini alitokemea kusikojulikna na mifuko hiyo.Pia alipotea tena na sh.80,000 zilizochangwa katika mkutano wa hadhara na Diwani wa kata hiyo kwa ajili ya kuunga mkono wananchi katika ujenzi huo.Pia Mkurugenzi ameongeza kuwa viongozi wa Serikali ya kijiji walikaa na kupitisha mitasari ili Mtendaji huyo aweze kuchukua fedha benki Sh.590,000 lakini mpaka sasa hazijulikani fedha hizo zilipo baada ya kuzitoa benki.
Hivyo ameamua k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More