Kaimu Rais atuliza hofu Simba - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kaimu Rais atuliza hofu Simba

Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba chini ya makamu mwenyekiti wake Stephen Ally imethibitisha kukamilika kwa zoezi la uchukuaji fomu za kugombea katika klabu hiyo huku anaekaimu nafasi ya Rais Salim Abdallah ‘Try Again akiwa hajachukua fomu.


Wadau wengi wa klabu ya Simba walikuwa wanaamini kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah angechukua fomu ya kugombea nafasi ya urais lakini haijawa hivyo. Baadhi ya mashabiki wamekuwa na wasiwasi kwamba nani anaweza kuipa mafanikio Simba kama ilivyokuwa chini ya Try Again.


Lakini Try Again amewatoa hofu wanasimba kwa kusema bado yupo ndani ya klabu hiyo na atashirikiana kwa karibu na viongozi watakaochaguliwa kwa kuwapa ushauri na kusimamia mambo mbalimbali akiwa nje ya uongozi.


“Kwa sasa Simba haihitaji kujadili mtu, kiongozi wa Simba kwa sasa sio mtu kiongozi wa Simba ni bodi kwa maana hatatizamwa mtu mmoja kwa sababu tunazungumzia kampuni”-Salim Abdallah (kushoto pichani juu), kaimu Rais Simba SC.


“Unapozungumzia kampuni haimaanishi ni... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More