Kajala- Sijavunja Ndoa Ya Pfunk - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kajala- Sijavunja Ndoa Ya Pfunk

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Kajala Masanja amekana tetesi zinazodai kuwa yeye ndio kapelekea ndoa ya Baba wa mtoto wake Pfunk kuvunjika.


Kajala na Pfunk walikuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi na kuzaa mtoto mmoja lakini baadae walikuja kuachana.


Siku za hivi karibuni wamedaiwa kurudiana licha ya kwamba Pfunk tayari ana mke na mtoto na mwanamke mwingine.


Kajala amekana kabisa kurudiana na Pfunk licha ya ukaribu wao waliounyesha siku za hivi karibuni hadi kupelekea kuambiwa amevunja ndoa ya Pfunk na mama watoto wake Samiraa.


Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Kajala amesema hajavunja ndoa ya watu Lakini pia hawezi kuacha kuwa karibu na Pfunk kwa sababu ni Baba wa mtoto wake na hayupo tayari kumtesa mtoto wake.Mimi sijavunja ndoa ya P Funk, yule ni mzazi mwenzangu, nimeishi naye miaka tisa, nimezaa naye mtoto (Paula) ambaye sasa hivi yupo kidato cha nne na ana miaka 16, si kosa mimi kupiga picha na mzazi mwenzangu“. 


 


The post Kajala- Sijavun... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More