KAKOLANYA NA DANTE WOTE WAPO FITI KABISA NA LEO WAMEFANYA MAZOEZI TAIFA STRAS - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAKOLANYA NA DANTE WOTE WAPO FITI KABISA NA LEO WAMEFANYA MAZOEZI TAIFA STRAS

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
PAMOJA na kushindwa kumalizia mechi jana kufuatia kuumia na kutolewa kwa machela, kipa wa Yanga Beno Kakolanya na beki Andrew Vincent ‘Dante’ leo asubuhi wote wamefanya mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Yanga SC jana ilijisogeza hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, lakini Kakolanya na Dante walitolewa kipindi cha pili baada ya kuumia.
Meneja wa Taifa Stars, Danny Msangi ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba wawili hao walipatiwa tiba nzuri jana baada ya mechi na hapana shaka wako tayari kuitetea nchi yao.  

Kipa Beno Kakolanya (katikati) na beki Andrew Vincent ‘Dante’ (kulia) wote wamefanya mazoezi Taifa Stars leo

“Beno na Dante wote wamefanya mazoezi leo asubuhi, kwa sababu baada ya mechi ya jana walipatiwa matibabu na wote wameamka vizuri,” amesema Msangi.
Taifa Stars watakuwa wageni wa Cape Verde ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More