KAKOLANYA NA YAHYA ZAYED HATARINI KUWAKOSA LESOTHO BAADA YA KUUMIA MAZOEZINI TAIFA STARS LEO AFRIKA KUSINI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAKOLANYA NA YAHYA ZAYED HATARINI KUWAKOSA LESOTHO BAADA YA KUUMIA MAZOEZINI TAIFA STARS LEO AFRIKA KUSINI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIPA Beno Kakolanya Yanga SC na mshambuliaji Yahya Zayed wa Azam FC wameibua hofu katika kambi ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars baada ya kuumia leo asubuhi mjini Bloemofontein nchini Afrika Kusini. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba Taifa Stars lo imeendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 dhidi ya Lesotho Novemba 18 mjini Maseru.
Na bahati mbaya katika mazoezi hayo, kipa Beno Kakolanya na mshambuliaji Yahya Zayed walipumzishwa baada ya kugongana, ingawa taarifa ya madaktari inasema wachezaji hao wataendelea na mazoezi kuanzia kesho.

Wachezaji wanaocheza nje wataanza kuripoti kambini Jumapili Novemba 11,2018. Wanaotarajiwa kuanza kuripoti ni Ramadhan Kessy(Nkamia,Zambia),Himid Mao (Petrojet,Misri),Rashid Mandawa(BDF,Botswana) na Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini) n waliobaki wataripoti kuanzia Novemba 12.
Taifa Sta... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More