KAMANDA MUSLIM SASA KUWANYAKUA MADEREVA WA SERIKALI WASIOFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMANDA MUSLIM SASA KUWANYAKUA MADEREVA WA SERIKALI WASIOFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

*Asema inasikitisha watumishi wa umma kupoteza maisha kwa ajali*Awataka waache kukimbia mwendo kasi, kupita magari bila uangalifu
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Fortunas Muslimu ametoa onyo kali kwa madereva wa Serikali ambao hawazingatii sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali zinazokatiza maisha watumishi wa umma ambao Serikali imetumia fedha nyingi kuwaandaa huku akisisitiza atakayevunja sheria atamnyakua tu na sheria kuchukua mkondo wake.
Amesisitiza umuhimu kwa madereva wote nchini wakiwamo hao wa Serikali kuhakikisha wanatii sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo zinaepuka iwapo sheria zitazingatiwa. Kamanda Muslim ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na Michuzi Blog iliyotaka kupata kauli yake kutokana na kuibuka kwa ajali za barabarani ambazo nyingi zinahusisha magari ya Serikali ambapo amesema jambo la msingi ni kuhakikisha madereva wanatii sheria zilizopo.
"Tumedhamiria kuchu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More