Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi wajifunza mengi TB3 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi wajifunza mengi TB3


WAJUMBE wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar imekiri kujifunza mambo makubwa katika ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3), imeelezwa.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambayo ilikuwa na ziara kwenye jengo hilo na Mhe. Mohammed Said (Mwakilishi wa Mpendae), amesema ujenzi wa jengo hilo ni fundisho tosha kutokana na kwenda kwa kasi tangu ujenzi wake uanze Juni 2013, tofauti na ujenzi wa jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume umechukua takribani miaka 10 tangu mwaka 2009 lakini hadi sasa lina asilimia 39 pekee.

Mhe. Said amesema TB3 ni jengo la kisasa kutokana na miundombinu yake ambayo mingi inaendeshwa kwa mifumo maalum, ikiwemo sehemu ya mizigo, ambayo inaendeshwa kupitia hatua tano.

“Katika ziara hii tumefarijika sana kwani tumejifunza mengi wenzetu walivyoweza kuufikisha mradi huu, kwa kweli tumechukua yote na tutakwenda kuishauri serikali namna bora ya kuend... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More