KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAVUTIWA NA MAFANIKIO YA TASAF MKOANI MTWARA. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAVUTIWA NA MAFANIKIO YA TASAF MKOANI MTWARA.

Na Estom Sanga- Mtwara 
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wameridhishwa na mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ambao umeleta hamasa kubwa kwa Walengwa wake kupambana na umaskini. 
Wajumbe wa Kamati hiyo ambao wametembelea kijiji cha Namela katika wilaya ya Mtwara ambako wamepata fursa ya kuonana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kushuhudia namna Walengwa hao wanavyotumia fursa za Mpango huo kujiletea maendeleo. 
Wakiwa kijijini hapo Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wamepata ushuhuda kutoka kwa baadhi ya Walengwa wa TASAF ambao wametumia fursa ya kuwepo kwenye Mpango huo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa mbuzi na Kuku wa Kienyeji kuhamasisha watoto wao kuhudhuria masomo huku wengine wakiboresha makazi yao na kununua vifaa vya umeme jua ( solar systems. 
‘’…….nimetumia fursa ya kuorod... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More