KAMATI YA BUNGE YAKABIDHI HATI ZA KWA WAKULMA-LINDI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMATI YA BUNGE YAKABIDHI HATI ZA KWA WAKULMA-LINDI

JOSEPH MPANGALA , NACHINGWEA LINDI
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za mitaa imekabidhi hati za Kimila za Umiliki ardhi Mia Moja{100} kwa wakazi wa kijiji cha Mbondo kilichopo Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi 
Ugawaji wa Hati hizo unakuja baada ya kujengewa Uwezo na Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania{MKURABITA} kwa kutoa mafunzo jinsi ya kupima ardhi kwa Halmashauri ya Nachingwea kwa lengo la kuongeza thamani ardhi hizo pamoja na kuondokana na Migogoro Mbalimbali inayotokana na Mipaka.
Menyekiti wa kamati hiyo Jason Rweikiza amesema ugawaji wa Hati utawezesha wakulima kuweza kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kuendeleza ardhi hizo kwa kulima kilimo kitakacholeta tija na mafanikio na hivyo kujiletea maendeleo.
“Tayari taasisi za kifedha zimeanza kukubali kupokea Hati hizi hivyo wakulima wananafasi kubwa ya kuweza kuendeleza mashamba yao kwa kulima kisasa zaidi na kujiletea maendeleo”amesema Rweikiza mwenyekiti wa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More