KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA MBEYA

 Jengo la Mahakama ya wilaya ya Rungwe na Mahakama ya Mwanzo ya Rungwe mjini likiwa katika hatua za awali za ujenzi. jengo hili linajengwa na Mkandarasi M/S Moladi Tanzania Ltd na kusimamiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi kama Mtaalam Mshauri. Ujenzi ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2017/2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili 2019. Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili leo mkoani Mbeya. Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi akiwaelezea waheshimiwa wabunge kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya Mahakama.  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza ufafanuzi juu ya mradi wa ujenzi wa Mahakama kutoka kwa Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania Bwn Khamadu Kitunzi (hayupo pichani) walipoongozana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea mradi huo.

 Jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole likiwa katika hatua za ukamilishwaji (finishing) Jengo hili linajengwa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More