KAMATI YA MAREKEBISHO YA KATIBA TASWA YAANZA MCHAKATO IKIOMBA USHIRIKIANO WA WANACHAMA WAKE ILI IKAMILISHE ZOEZI MAPEMA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMATI YA MAREKEBISHO YA KATIBA TASWA YAANZA MCHAKATO IKIOMBA USHIRIKIANO WA WANACHAMA WAKE ILI IKAMILISHE ZOEZI MAPEMA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imeanza mchakato kuhusu marekebisho ya katiba ya chama hicho kama ilivyoagizwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT). 
Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari leo, Katibu Mkuu TASWA Amir Mhando amesema kwamba, Kamati ya Katiba inayoongozwa na Mwenyeketi wa zamani wa chama hicho, Boniface Wambura inaomba ushirikiano wa waandishi wote wa habari za michezo nchini kufanikisha jukumu hilo kwa wakati uliopangwa na BMT,  ili chama kifanye Uchaguzi Mkuu na kupata viongozi wapya. 
Mhando amesema kutokana na suala la muda kuwa mfupi, Kamati imeandaa utaratibu wa kupokea maoni ya waandishi wa habari za michezo kwa njia mbalimbali kabla ya kuiwasilisha kwa Kamati ya Utendaji ya TASWA kupata baraka na kuitisha mkutano wa pamoja wa wadau kupitisha rasimu ya katiba hiyo. 
Katibu Mkuu TASWA, Amir Mhando (kulia) akiwa na Mwenyeketi wa chama hicho, Juma Pinto (kushoto)

"Wadau wenye... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More