KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KIGOMA YATEKETEZA SHEHENA YA NGUO ZINAZOFANANA NA SARE YA JESHI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KIGOMA YATEKETEZA SHEHENA YA NGUO ZINAZOFANANA NA SARE YA JESHI.

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
KAMATI ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma imeteketeza jumla ya nguo 1947 zinazofanana na sare za jeshi zilizokamatwa kwenye kambi za wakimbizi za Mtendeli na Nduta Wilayani Kibondo.
Akiongea na wananchi baada ya kuteketeza nguo hizo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa nguo hizo zinazofanana na sare za jeshi ziliingizwa kambini na Mkurugenzi wa shirika Danish refugees council kwaajili ya kugawa kwa wakimbizi katika kambi ya Nduta na Mtendeli Wilayani Kibondo.
Alisema Viongozi wa serikali ya Wilaya walipata taarifa kutoka kwa mkuu wa makazi ya wakimbizi kuna nguo zimeingizwa kambini zinazofanana na sare za jeshi kwaajili ya kuwagawia wakimbizi kama msaada wa nguo."Baada ya kupata taarifa wakazifanyia kazi kwa haraka na wakafanikiwa kuzidhibiti na hakuna mkimbizi hata mmoja aliyefanikiwa kupewa"alisema
Anga amewataka wananchi kuacha tabia kutumia nguo zinazofan... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More