KAMATI ZA USIMAMIZI WA MAAFA ZASHAURIWA KUWA NA MPANGO WA KUJIANDAA KUKABILIANA NA MAAFA. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMATI ZA USIMAMIZI WA MAAFA ZASHAURIWA KUWA NA MPANGO WA KUJIANDAA KUKABILIANA NA MAAFA.

Na OWM, SUMBAWANGA.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa, imezishauri Kamati za Usimamizi wa maafa nchini kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa kuwa na mpango wa Kujiandaa na kukabili maafa ili kuwa na uwezo wa  utayari wa kujiandaa na kukabili maafa kwa ufanisi.
Akiongea wakati wa mafunzo kwa Kamati ya Usimamizi ya Maafa ya Mkoa wa Rukwa, juu ya Usimamizi wa Maafa kwa Mujibu wa Sheria ya Maafa Na. 7 ya mwaka 2015, Mkurugenzi Msaidizi (Utafiti na Mipango), Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashir Taratibu, alifafanua kuwa Mpango huo ni muhimu kwa kuwa huainisha majukumu na hatua zitakazochukuliwa na Kamati za  maafa kuanzia  ngazi ya kijiji, wilaya na mkoa pamoja na wadau wengine wa maafa.
“Ili kuweza kukabiliana na maafa pindi yanapotokea na kuhakikisha kuwa wanazuia au kupunguza athari za maafa yanapotokea kwa ufanisi tumeishauri kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa wa Rukwa katika bajeti ijayo watenge bajeti  kwa ajili ya maafa,  pia wabuni mbinu za upatikanaji wa rasilimali zinazohi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More