KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI ATEMBELEWA NA MKURUGENZI MKUU TAKUKURU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI ATEMBELEWA NA MKURUGENZI MKUU TAKUKURU

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman jana katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili.Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa. Vilevile Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo. “Nimejifunza mengi laki... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More