KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AASA JAMII KUACHA KUTENDA UHALIFU ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AASA JAMII KUACHA KUTENDA UHALIFU ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI

Na Lucas Mboje, Iringa;KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Magereza nchini, Phaustine Kasike ametoa rai kuwa ili kupunguza msongamano magerezani ni vema jamii ikaacha kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu hapa nchini.Rai hiyo imetolewa leo na Kamishna Jenerali Kasike wakati akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabari wa Mkoani Iringa kuhusu madai ya uwepo wa msongamano wa wafungwa katika magereza mbalimbali yaliyopo nchini ambapo ameeleza kuwa si kweli kwamba magereza yote yana msongamano bali msongamano uliopo magerezani ni kwenye baadhi ya magereza yenye kuhifadhi mahabusu.Amesema suala la msongamano limekuwa ni tatizo kubwa ambapo takwimu za Jeshi la Magereza zinaonesha kuwa idadi ya mahabusu waliopo magerezani ni wengi na hali hiyo inatokana na wingi wa matukio ya uhalifu kwenye eneo husika na kule ambako hakuna uhalifu mwingi basi nako kwenye magereza hakuna msongamano mkubwa wa wafungwa/mahabusu.Ameongeza kuwa Jeshi la Magereza litaendelea kushirikiana na vyombo vya haki jinai ikiwemo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More