KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKEA MISAADA YA KIBINADAMU YA WAFUNGWA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI


Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Ndg. Charles Shang’a mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya wafungwa leo Septemba 8, 2018.
Na Deodatus Kazinja, Moshi
Wito umetolewa kwa Asasi mbalimbali za kiraia nchini kujitokeza kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazoweza kulikwamisha katika kutoa huduma muhimu za wafungwa magerezani  kutokana na ufinyu wa bajeti. 
Hayo yamesemwa leo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Phaustine Kasike katika hafla ya kupokea msaada wa Kibinadamu uliotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ  iliyofanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga mjini Moshi jana Septemba 8, 2018.
“Ni ukweli usiopingika kuwa Jeshi la Magereza limekuwa likishindwa kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa ... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More