KAMISHNA MKUU WA TRA AFUNGUA FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMISHNA MKUU WA TRA AFUNGUA FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI

Na Veronica Kazimoto -Dar es Salaam

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amefungua fainali za mashindano ya kumi na moja (11) ya vilabu vya kodi katika Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es salaam na Pwani yaliyofanyika leo katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa, Kichere amesema lengo la mashindano hayo ni kuwafundisha wanafunzi uzalendo na kukuza uelewa wao juu ya masuala mbalimbali ya kodi ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari. "Haya mashindano yanafanyika kama sehemu ya kujenga uzalendo kwa wanafunzi wetu ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na hatimaye waweze kulipa kodi kwa hiari maana tunasema samaki mkuje angali mbichi," alisema Kichere.

Ameongeza kwa kusema kuwa, "Sisi Mamlaka ya Mapato Tanzania tunasema kwamba elimu ndio kitu muhimu sana kwasababu watu wakielewa umuhimu wa kulipa kodi, tutakusanya kodi nyingi zaidi ambazo hutumika kat... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More