KAMPASI ZA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KUSHINDANISHWA KIUTENDAJI ILI KUBORESHA HUDUMA ZAKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMPASI ZA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KUSHINDANISHWA KIUTENDAJI ILI KUBORESHA HUDUMA ZAKE

Serikali imepanga kushindanisha huduma zinazotolewa na kampasi za Chuo cha Utumishi wa Umma nchini ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa chuo hicho, lengo likiwa ni kuboresha huduma zinazotolewa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziarayake ya kikazi mkoani Tabora ya kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, kampasi ya Tabora ili kukagua utekelezaji wa miradi na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, kampasi zitakazoshindanishwa ni za Dar es Salaam, Mtwara, Tabora, Singida, Tanga na Mbeya ambapo ameweka bayana kuwa, kampasi itakayoshinda katika utoaji wa huduma bora   itapewa tuzo.“Utawekwa utaratibu ambao utashindanisha kampasi zote kwa kuzingatia vigezo stahiki ili kumpata mshindi anayestahili" Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, mashindano hayo yatakuwa ni chachu ya kuongeza ufanisi wa utendaji kaz... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More