KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAMPENI YA KUMTUA MAMA NDOO INAENDELEA KUTEKELEZWA KAGERA


Naibu Waziri wa Maji  Jumaa Aweso anaendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera akiwa tayari amemaliza Ziara ya kutembelea, Kukagua na Kuzindua Miradi ya Maji ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mnamo  Januari 11,Magufuli Mh. Aweso ametembelea na kukagua mradi wa Maji katika Kata ya Ibwera eneo la Rugaze ambapo mradi huo tayari unafanya kazi na unauwezo wa kuhudumia Wananchi 500 wa Vijiji jirani.
Kisha Mh. Aweso ameendelea na Ziara hiyo katika kata ya Kibirizi ambapo ameweza kuzindua Mradi mpya wa Maji wenye zaidi ya Shilingi Milioni 500. Mradi huo uliopo katika Kijiji cha Kibirizi umeanza kuhudumia takribani vitongoji 10 kati ya 14 vinavyopatikana ndani ya Kijiji hicho na huku juhudi zikiendelea kufanyika kuwafikia wananchi wengine.
Kwa upande mwingine mradi wa Maji Kijiji cha Kyamulalile na Mashule kwa sasa haufanyi kazi kutokana na athali ya tetemeko licha ya kuwa tayari Halmashauri imekwishatenga zaidi ya shilingi milioni 80, kwa ajili ya Ukarabati na tayari mkandarasi amea... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More