Kampuni ya Vodacom yalipa Zaidi ya TZS bilioni 54.5 kama gawio kwa Wanahisa - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kampuni ya Vodacom yalipa Zaidi ya TZS bilioni 54.5 kama gawio kwa Wanahisa


· Vodacom yatoa taarifa ya ongezeko la faida kwa mwaka kufikia TZS billioni 90.2


 Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC imetangaza faida ya mwisho wa mwaka ya kiasi cha TZS bilioni 90.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia mwezi Machi mwaka huu.

Wakati huo huo Kampuni ya Vodacom ambayo ina mtandao wenye kasi zaidi nchini inajivunia thamani iliyojitengenezea katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ikiwemo TZS bilioni 54.5 ambazo zimelipwa kama gawio kwa wanahisa.

Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma ambayo yanafikia TZS bilioni 1018.9, ambayo yamesababishwa na kukua na kuimarika kwa mapato yatokanayo na huduma za M-pesa, ununuzi wa Intaneti (Bando) na mapato yatokanayo na ujumbe wa simu. Kampuni ya Vodacom imepata wateja wapya wapatao milioni 1.2 katika mwaka huu wa fedha jambo ambalo linaongeza idadi yake ya wateja kufikia milioni 14.1.

Katika mwaka huu wa fedha kampuni ya Vodac... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More