KARIA AMVUA SANGA UENYEKITI WA BODI YA LIGI, ASEMA HANA SIFA...KIDAU APEWA 'ULAJI' RASMI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KARIA AMVUA SANGA UENYEKITI WA BODI YA LIGI, ASEMA HANA SIFA...KIDAU APEWA 'ULAJI' RASMI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Sheria na Katiba ya kumsimamisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga baada ya kukosa sifa za Uenyekiti wa Bodi hiyo. 
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia amesema kwamba hatua imefuatia Mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga kusema bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

Rais wa TFF, Wallace Karia (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam

Karia amesema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anatakiwa awe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu, Sanga amepoteza sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa bodi hiyo.
"Tulipokea barua Julai 12 kutoka klabu ya Yanga ikidai kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo, wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Lig... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More