KARIA AWAPA YANGA SAA 48 KUTENGUA KAULI YA KUJITOA KOMBE LA KAGAME, VINGINEVYO… - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KARIA AWAPA YANGA SAA 48 KUTENGUA KAULI YA KUJITOA KOMBE LA KAGAME, VINGINEVYO…

Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameutaka uongozi wa klabu ya Yanga kutoa jibu linaloeleweka hadi kufika Jumapili juu ya kujitoa kwao kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Kauli hiyo ya Karia leo, inafuatia Yanga kuiandikia barua TFF kuwaarifu kutoshiriki michuano hiyo kutokana na kubanwa na ratiba ya mashindano mengine.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Rais Karia amesema kwamba sababu walizozitoa Yanga hazina mashiko, kwani hata timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo nazo zina ratiba ngumu pia.
“Sababu walizozitoa Yanga juu ya kutoshiriki michuano ya Kagame hazina mashiko, maana si Yanga peke yao ambao ratiba imewabana na ukiangalia hiyo michuano ya Shirikisho Afrika hata Gor Mahia pia wapo, mashindano ya Sportspesa Super Cup ambayo mpaka hivi sasa Gor Mahia wapo na wanacheza fainali Jumapili na Simba,” amesema Karia na kuongeza; “Hivyo kabla hata hatujalipeleka suala hili... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More