KARIA: BADO TUNAENDELEA NA MAZUNGUMZO NA VODACOM WAENDELEE KUDHAMINI LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KARIA: BADO TUNAENDELEA NA MAZUNGUMZO NA VODACOM WAENDELEE KUDHAMINI LIGI KUU

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM 
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwamba bado wapo kwenye mazungumzo na kampuni ya Vodacom juu ya mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwenye mahojiano maalum mjini Dar es Salaam, Karia amesema kwamba anashangazwa na wanaosema kuanzia msimu ujao Ligi Kuu haitakuwa na mdhamini mkuu.
“Inafahamika kila mkataba wa Vodacom unapofikia tamati mazungumzo huwa mazito na ya mvutano hadi makubaliano yanafikiwa dakika za mwisho kabla ya Ligi Kuu kuanza, watu wavute subira, bado tunaendelea na mazungumzo,”amesema Karia. 
Pamoja na hayo, Karia amesema kwamba kuna uwezekano Ligi Kuu ikawa na wadhamini zaidi ya wawili msimu huu, kwani mazungumzo yanaendelea vizuri na makampuni mbalimbali.

Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) amesema bado wapo kwenye mazungumzo na Vodacom waendelee kudhamini Ligi Kuu

Ligi Kuu msimu wa 2018-2019 inatarajiwa kuanza Agosti 22 na hadi sasa ni Benki ya Biashar... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More