KARIA, KIDAU WAKOSEKANA OFISINI WAMBURA AKIKABIDHI BARUA YA KUREJESHWA MADARAKANI NA MAHAKAMA LEO ASUBUHI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KARIA, KIDAU WAKOSEKANA OFISINI WAMBURA AKIKABIDHI BARUA YA KUREJESHWA MADARAKANI NA MAHAKAMA LEO ASUBUHI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura leo amekabidhi barua ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kutengua maamuzi ya Kamati za Maadili za shirikisho hilo kumfungia maisha kujihusishan na mchezo huo.
Wambura amekabidhi barua hiyo asubuhi ya leo ofisi za TFF makao makuu, Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam na akasema atapeleka nakala Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). 
Hata hivyo, Wambura hakufanikiwa kumkuta yeyote kati ya viongozi wakuu wa TFF, Rais, Wallace Karia au Katibu Mkuu, Wilfred Kidau hivyo barua hiyo akaikabidhi kwa maofisa wengine aliowakuta ambao walisiani kudhihirisha wameipokea.
Michael Wambura akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisi za TFF, Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam 

Na Wambura akasema baada ya kukabidhi barua huyo anarejea rasmi kazini katika wadhifa wake wa Makamu wa Rais wa TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mara (FAM).
“Sihitaji kuwaomba kurudi ofisini, mimi nilic... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More