KASEJA ASEMA YANGA ILIWASAIDIA KUWAPIGA STAND UNITED KIULAINI JANA, ATABIRI KMC ITATISHA BAADAYE WATU HAWATAAMINI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KASEJA ASEMA YANGA ILIWASAIDIA KUWAPIGA STAND UNITED KIULAINI JANA, ATABIRI KMC ITATISHA BAADAYE WATU HAWATAAMINI

Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa KMC, Juma Kaseja amesema kwamba walifanikiwa kuwafunga kwa urahisi Stand United jana kwa sababu walikuwa wana uchovu baada ya kutumia nguvu nyingi kwenye mechi dhidi ya Yanga SC.
Stand United ilichapwa 2-0 jana Uwanja wa Uhuru na KMC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ikitoka kuchapwa 4-3 na Yanga SC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo uliotangulia.
Na akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mchezo wa jana, Kaseja alisema kwamba walicheza kwa kushambulia kwa sababu walijua wapinzani wao watachoka kwa kuwa wametoka kucheza mechi kubwa dhidi ya Yanga.

Juma Kaseja amesema waliifunga kwa urahisi Stand United jana kwa sababu walikuwa wana wa mechi na Yanga SC

“Tunamshukuru Mungu tumepata ushindi wa kwanza, lakini ukiangalia hata mechi tuliyopoteza juzi na Singida tulitengeneza nafasi nyingi tukakosa. Leo mwalimu alituambia tupeleke mbele na tushambulie kwa sababu wametoka kucheza mchezo mkubwa na Yanga watakuwa wametumia nguvu nyingi sana, ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More