Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kasulu Mmejipanga- Jafo Alonga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa la Moyoni kwa kuwaeleza Mkuu wa Wilaya ya Kasulu pamoja na viongozi wenzake kwamba wamejipanga vyema katika kuwatumikia wananchi wa Kasulu. 
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo ya kufurahishwa baada ya kutembelea miradi minne ya sekta ya afya pamoja na barabara wilayani humo na kuridhishwa Sana na usimamizi mzuri wa miradi Hiyo. Miradi aliyo ikagua ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Lami katika Halmashauri ya mji wa Kasulu, ukarabati wa Hospitali ya Mji Kasulu na Kituo cha Afya Kiganamo. 
Pia katika halmashauri ya wilaya Kasulu Waziri Jafo alifanikiwa kukagua kituo kimoja cha Afya cha Rusesa ambacho ni moja ya kituo cha afya kati ya vituo vya afya vitatu vilivyojengwa na Serikali katika halmashauri hiyo. 
Katika Zara hiyo waziri Jafo alimshukuru sana Mhe. Daniel Nsanzugwako Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini na Mhe. Vuma Mbunge wa Jimbo la Kasulu vijijini kwa kufikisha kilio cha wananchi wao serikalini hadi serikali imefanikisha kutekeleza miradi ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More