KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mwl. Raymond Mwangwala atikisa Jang'ombe - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mwl. Raymond Mwangwala atikisa Jang'ombe

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl. Raymond Mwangwala amewasihi wananchi wa jimbo la Jang’ombe hasa vijana kumchagua kwa kura za ndio mgombea wa tiketi ya CCM Ramadhan Hamza Chande.  Wito huo ameutoa leo alipokuwa akimnadi na mgombea wa CCM Jimbo la Jang’ombe huko katika Mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika Tawi la Kidongo Chekundu Unguja. Amemtaja mgombea huyo wa CCM kuwa ni mgombea pekee mwenye sifa na vigezo vya kuleta mabadiliko chanya ya maendeleo katika Jimbo hilo.  Mwl. Raymond amesema viongozi mbali mbali wa CCM katika Jimbo la Jang’ombe wametekelea kwa ufanisi miradi ya maendeleo na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto sugu za jimbo. Pia ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya saba inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2016 hatua ambazo zinastahiki kuungwa mkono na wananchi wote hasa wa Jim... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More