Katibu Mkuu wizara ya Fedha Doto James awataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta (TEMCO) Kibaha - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Katibu Mkuu wizara ya Fedha Doto James awataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta (TEMCO) Kibaha

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James amewataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta yaliyopo katika kiwanda cha kuunganisha matrekta ambacho kinamilikiwa na Serikali kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Amesema kuwa matrekta hayo yanaubora wa hali ya juu na kuwahakikishia wananchi watakaoyanunua matrekta hayo kutokuwa na hofu kwani uingizwaji wake Serikali inahusika moja kwa moja.Katibu James aliyasema hayo Kibaha mkoani Pwani wakati akikabidhi matrekta kumi kwa Chuo cha kilimo Sokoine (SUA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi I littles na Rais Dkt.John Magufuli baada ya kufanya ziara chuoni hapo .
Alifafanua rais alipofanya ziara chuoni hapo alihaidi mambo mawili la kutoa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ahadi ambayo tayari imetekelezwa na jana amekamilisha ahadi ya kukabidhi matrekta hayo." Ninawataka kwenda kutumia vizuri matrekta haya na kuyafanyia matengenezo iwapo yatahitaji matengenezo kwani sisi watanza... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More