Katibu Mtendaji BASATA apewa tuzo ya kimataifa kutoka Marekani, apongezwa kwa kukuza sanaa nchini - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Katibu Mtendaji BASATA apewa tuzo ya kimataifa kutoka Marekani, apongezwa kwa kukuza sanaa nchini

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza wikiendi hii amekabidhiwa tuzo maalum na Mkurugenzi wa taasisi kutoka Marekani ya The African Film Festival Bw. Kelechi Eke katika kuthamini mchango wake wa kukuza sekta ya Sanaa nchini.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza kulia akikabidhiwa cheti na tuzo hiyo.

Tukio hilo la kukabidhiwa tuzo hiyo limeshuhudiwa na Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Wizara yenye dhamana na Sanaa Mhe. Juliana Shonza (MB), limefanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ulioko jijini Dar es Salaam na limeenda sambamba na uzinduzi wa programu ya “Act na Monalisa” inayoratibiwa na kuendeshwa na Msanii maarufu nchini wa Filamu Yvone Cherrie maarufu kwa jina la Monalisa inayolenga kusaka vipaji vya waigizaji wa filamu wa kike nchini.


Monalisa pia ni balozi wa Kampuni hiyo ya African Film Festival hapa nchini. Tanzania.


The post Katibu Mtendaji BASATA apewa tuzo ya kimataifa kutoka Marekani, apongezwa ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More