Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo ampongeza msanii Monalisa baada ya kushinda tuzo hii nchini Uganda - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo ampongeza msanii Monalisa baada ya kushinda tuzo hii nchini Uganda

Leo tarehe 08/11/2018 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo amempongeza na kumtaka Mwanatasnia wa Filamu Bi. Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda.Pongezi hizo amezitoa leo ofisini kwake Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam alipokutana na Muigizaji huyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.


Bi. Fissoo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii.“Wewe ni mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kuithamini na kuiheshimu kazi yako, niwakumbushe Wadau wote kujifunza yale mambo chanya kutoka kwako” Alisema Fissoo.


Kwaupande wake Monalisa alimshukuru Katibu Mtendaji Bi. Fissoo kwa kuendelea kuwapa ushrikiano akiwepo yeye mwenyewe na Bodi kuwa sehemu... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More