KAULI YA MBWANA SAMATA BAADA YA POLISI KUMSHAMBULIA MWANDISHI WA HABARI DAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAULI YA MBWANA SAMATA BAADA YA POLISI KUMSHAMBULIA MWANDISHI WA HABARI DAR

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAKATI Watanzania mbalimbali wakitoa matamko ya kulaani kitendo cha Mwandishi wa habari wa Wapo Redio Silas Mbise kushambuliwa na Polisi katika mechi kati ya Simba na Asante Kotoko Siku ya Simba Day mchezaji wa kimataifa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’Mbwana Samata amesema kitendo hicho si cha kiungwana.
Samata ametoa kauli hiyo kutokana na kusambaa kwa video inayoonesha namna ambavyo mwandishi huyo akishambuliwa licha ya kujisamilisha.Hivyo kutokana na video hiyo Samata kupita ukurasa wake wa Tweet ameelezea kusikitishwa na shambulio hilo.
Samata amesema hivi “Sio kitendo cha kiungwana askari kupiga mwandishi katika eneo la michezo , mpira ni mchezo unaoleta amani sio kuvunja amani.”.Wakati Samata akitoa kauli hiyo tayari leo mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linalaani vikali tukio hilo linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandishi huyo.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More