KAZI YANGU NI KUWATUMIKIA WANAKAGERA UTUMISHI ULIOTUKUKA-RC KAGERA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KAZI YANGU NI KUWATUMIKIA WANAKAGERA UTUMISHI ULIOTUKUKA-RC KAGERA

Na Editha Karlo,Blobu ya Jamii Kagera.

MKUU wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wanakagera kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya ya kikazi aliyoanza ili kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake.

Gaguti ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa halmashauri ya Bukoba baada ya kukabidhiwa ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Meja Jenerali Salum Kijuu na kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu.

Alisema nafasi yake ni kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake kwa wanakagera ili kuhakikisha Mkoa wa Kagera unasonga mbele."Ni wajibu wangu kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wangu na nina imani kubwa tutashirikiana na viongozi wenzangu na nitatoa ushirikiano wakati wowote nipo tayari"alisema Mkuu huyo wa Kagera

Gaguti alisema Mkoa wa Kagera ni Mkoa ambao upo mpakani na unapakana na nchi karibia tatu hivyo aliwataka wananchi wa Mkoa huo kutumia fursa hiyo kuuza mazao ili kuufanya Mkoa kuwa wa viwanda na wenye neema.

Mk... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More