KENYA: MAAFISA POLISI WAWILI WATIWA NGUVUNI KWA KULAZIMISHA KUJAZIWA MAFUTA BURE - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KENYA: MAAFISA POLISI WAWILI WATIWA NGUVUNI KWA KULAZIMISHA KUJAZIWA MAFUTA BURE

Kenya

Taarifa kutoka katika mji wa kisumu nchini Kenya zinasema kuwa maafisa polisi wawili wamekamatwa kwa kosa la kuzalimisha kujaziwa mafuta kwa nguvu. 
Maafisa hao walifika kwenye kituo cha mafuta kilichopo Kisumu muda wa saa 7 usiku wakiwa wanaendesha Pikipiki na kumkuta mwendesha magari ya mafuta akishusha mafuta kwenye kituo hicho na kutaka wafahamu ni kwa nini anafanya hivyo usiku ule
Kwa mujibu wa maelezo yaliyopo Polisi, maafisa hao walianza kumpiga dereva huyu wa gari la mafuta pamoja na muhudumu wa kituo hicho huku wakimuamirisha dereva huyo awawekee mafuta kwenye pikipiki zao
Madereva bodaboda wanaoegesha pikipiki zao karibu na kituo hicho cha mafuta waliposhuhudia hayo yakitokea walipiga simu polisi na kuomba msaada na ndipo polisi walipofika hapo na kukamata maafisa hao
Maafisa hao waliokamatwa siku ya Alhamisi usiku ni Valentine Ochieng na Julius Oduor na walipelekwa kwenye kituo cha Polisi kilichopo Kisumu wakisubiri tarabibu zaidi. ... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More