Kenya yaichakaza Mauritius 5-0, Tanzania U23 yaanza kwa kipigo - Mwanaspoti | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kenya yaichakaza Mauritius 5-0, Tanzania U23 yaanza kwa kipigo

Nairobi, Kenya. Kenya imeanza vyema kampeni yake ya kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON U23) na michezo ya Olimpiki 2020, kwa wachezaji chini ya umri wa miaka 23, kwa kuichakaza Mauritius 5-0, katika mchezo mkali uliomalizika muda mfupi uliopita, ugani Moi Kasarani. huku timu ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 23 ikipoteza mchezo wake wa kufuzu AFCON nchini burundi baada ya kufungwa mabao 2-0.
Mabao kutoka kwa Johnstone Omurwa (dk 11), James Mazembe (dk 13), Piston Mutamba (dk 36), Sydney Lokale (dk 55) na Nahodha Joseph Okumu (dk 87), yalitosha kumfanya kocha wa Kenya U23, maarufu kama Emerging Stars, Francis Kimanzi atabasamu na kupeleka simanzi katika kambi ya Mauritius, kabla ya mechi ya marudiano , itakayopigwa majuma mawili yajayo, nchini Mauritius.
Kikosi cha Kenya U23: Brian Bwire (GK), 2. Nahodha Joseph Okumu, Yussuf Mainge, Johnstone Omurwa, David Owino, Teddy Osok, Ovella Ochieng, Ibrahim Shambi, Chrispinus Onyango, James Mazembe, Pistone ... Continue reading ->


Source: MwanaspotiRead More