KENYA YAZUIA UINGIZAJI WA VIGAE, HALI INAYOSABABISHA HASARA KWA WAWEKEZAJI KUTOKA TANZANIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KENYA YAZUIA UINGIZAJI WA VIGAE, HALI INAYOSABABISHA HASARA KWA WAWEKEZAJI KUTOKA TANZANIA


NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
KIWANDA cha Goodwill Tanzania Ceramic co.ltd kilichopo Mkiu ,Mkuranga Mkoani Pwani, kinachozalisha vigae kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa soko baada ya nchi ya Kenya kuzuia uingizwaji wa bidhaa hiyo. Hatua hiyo iliyochukua nchi hiyo inasababisha shehena kubwa ya vigae kurundikana kwenye magodauni na kupata hasara.
Meneja uajiri katika kiwanda hicho ,Msafiri Figa aliyasema hayo wakati kamati ya siasa mkoa, ilipokwenda kutembelea kuona shughuli za uzalishaji kiwandani hapo. Alisema ,walikuwa wakitegemea soko la Kenya zaidi kutokana na kupata oda nyingi kutoka kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo . Figa alisema ,kipindi kiwanda kinaanza lengo lao ilikuwa kuzalishaji mita za mraba 80,000 sawa na vigae 800,000 kwa siku lakini kwa sasa tangu waanze kuzalisha wanazalisha vigae 600,000 kwa siku.Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (wa nne kulia) akiangalia kigae wakati kamati ya siasa mkoani Pwani ilipokwenda kutembelea kiwanda cha Goodwill ceramic co.ltd Mkuranga na kukuta shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda katika kiwanda hicho kwa kukosa soko.Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akiongea jambo na MNEC Kibaha ,Hajji Jumaa , wakati kamati ya siasa mkoani Pwani ilipokwenda kutembelea kiwanda cha Goodwill ceramic co.ltd ,Mkuranga na kukuta shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda katika kiwanda hicho kwa kukosa soko.
"Kadri siku zikienda imekuwa tukizalisha mita za mraba 50,000 kutokana na tatizo soko ,tulilenga soko la ndani kwa asilimia 60-70 na soko la nje asilimia 30-40 lakini imebadilika na kuwa soko la ndani 30-40 nje ikawa asilimia 60-40 huku tukizalisha mita za mraba ya vigae 30,000-20,000 kwa siku " .
Figa alielezea, wana wafanyakazi 900 kutoka Tanzania,ajira zisizo za moja kwa moja 2,000-3,000 na wachina 60 ambao ni pamoja na wataalamu mbalimbali.Nae mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema hali iliyopo ni hatari kwani inakwenda kuuwa viwanda na kuweka hofu ya kuzima ndoto yetu.
"Mwaka mmoja na nusu uliopita eneo hili lilikuwa pori ambapo sasa kuna kiwanda kikubwa ambacho kinatengeneza ajira na kuliingizia mapato Taifa"Ndikilo alieleza ,tatizo la ukosefu wa soko sio la kubeza ,sio la masihala,hivyo amekiomba chama kisimamie hilo. Alisema ,wapo wafanyabiashara wanaagiza vigae China suala hili linakandamiza wawekezaji wa ndani .Mfanyakazi katika kiwanda cha Goodwill ceramic co.ltd ,Mkuranga akipakia mabox ya vigae, wakati kamati ya siasa mkoani Pwani ilipokwenda kutembelea na kukuta shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda katika kiwanda hicho kwa kukosa soko .
"Wapo watendaji serikalini wanaotoa vibali kwa wanyabiashara kuagiza nondo Uturuki na vigae China,Spain na wengine kuchukua chuma nje hivyo kuna kila sababu kuliangalia tatizo hilo" alisisitiza Ndikilo.Alisema, serikali inafanya kazi lakini baadhi ya watendaji wanasababisha tatizo hili kwa maslahi binafsi.
Kwa upande wake ,mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ramadhani Maneno alisema ,wataishauri serikali kupitia wizara husika kuanza kutazama muundo wa sera ya masoko . Alisema, wataangalia namna ya kukaa na wizara ya viwanda na biashara ,wizara ya fedha kuweka masharti kwa wafanyabiashara ,"Kuwawekea masharti bila kuwaonea haya kuwa ukiwa Tanzania hakuna budi kutumia bidhaa zinazozalishwa viwanda vya ndani.
"Duniani kote ukizalisha lazima utegemee soko hivyo kama ukizalisha bila kuuza ni kazi bure kwani uzalishaji ukipungua kwa kukosa soko ajira zitapungua na kukatisha tamaa wawekezaji" alibainisha Maneno.Shehena ya vigae iliyorundikana katika kiwanda cha vigae cha Goodwill Ceramic co.ltd ,Mkiu Mkuranga mkoani Pwani kwa kukosa soko .(picha na Mwamvua Mwinyi).


Source: Issa MichuziRead More