KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametaka kero ya maji kwa wakazi wa Mtoni itatuliwe haraka iwezekanavyo mara baada kujionea hali huduma ya maji kwa wananchi. 
Amezungumza hayo katika muendelezo wa ziara yake ya kusiskiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam, na kuitaka DAWASA itafute suluhisho la kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, ukizingatia uwepo wa chanzo cha maji na mtambo wa kusafishia maji katika eneo la Mtoni.

Profesa Mbarawa amesema haoni sababu ya wananchi hao kukosa maji kwa kuwa kuna chanzo cha maji cha uhakika, kinachohitajika ni kuweka mkakati mzuri wa ujenzi wa miundombinu itakayofikisha maji kwa wananchi kwa kuwa chanzo kipo. Akiwa kwenye Mtaa wa Mashine ya Maji, Profesa Mbarawa amekutana na kero ya maji kutoka kwa wananchi ambao wamesema maji wanayotumia yanayotoka kwenye kisima usalama wake ni mdogo, kumuomba Waziri wa Maji awatatulie changamoto hiyo.

Aidha, wamemuomba Waziri wa Maji aipatie ufumbuzi changamoto ya kisima kilichochimbwa na Ha... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More