KESI YA KUMILIKI MALI KULIKO UWEZO WAKE INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU YAUNGURUMA TENA MAHAKAMANI,ALIYEMUUZIA KIWANJA ATOA USHAHIDI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KESI YA KUMILIKI MALI KULIKO UWEZO WAKE INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU TAKUKURU YAUNGURUMA TENA MAHAKAMANI,ALIYEMUUZIA KIWANJA ATOA USHAHIDI

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mkataba wa mauziano ya kiwanja kati ya aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai, na aliyemuuzia Abubakar Hamis uliandikwa Sh.milioni 60 lakini walipewa Sh.milioni 80 ili wapate ahuweni ya kodi.

Hamis (46), ambae ni mkazi wa Boko, na shahidi wa 20 katika kesi utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato, inayomkabili Gugai na wenzake wanne.

Akiongozwa na Wakili wa serikali kutoka (Takukuru) Awamu Mbagwa, kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, shahidi huyo amedai mahakamani hapo  kuwa Gugai ni jirani yake na amewahi kufanya nae biashara.

Amedai walifanya makubaliano baina ya familia ya Gugai ya kuuziana kiwanja namba 64 kilichopo kitalu C eneo la Boko Ununio Dar es Salaam, kwa Sh. milioni 80 na malipo yalifanyika kwa fedha taslimu ambapo mwanasheria wake alienda kuandaa mkataba na walipofika nyumbani kwake jioni aliwapa na kuusoma kisha akawakabidhi fedha.

Shahidi ameendelea ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More