KIGWANGALLA AFUTURISHA WABUNGE DODOMA, ASISITIZA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KIGWANGALLA AFUTURISHA WABUNGE DODOMA, ASISITIZA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefuturisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake yaliyopo Area D Jijini Dodoma.
Futari hiyo ilihudhauriwa na wabunge mbalimbali wa chama tawala CCM na wa vyama vya upinzani wakiongozwa na Spika, Job Ndugai na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson.
Dkt. Kigwangalla aliwashukuru wabunge wote waliohudhuria hafla hiyo na kusema kuwa imelenga kudumisha upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa uliopo baina ya wabunge hao bila ya kujali mipaka ya vyama vyao hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
"Nimefarijika sana kuwapokea waheshimiwa wabunge wenzangu hapa nyumbani kwangu, ninawashukuru sana kwa kuja maana shughuli ni watu, tuliandaa futari nyingi kwa ajili ya wabunge wote, sasa msingefika tungepata mtihani ni wapi pa kuipeleka. "Hafla kama hii ya Iftar inatuunganisha sisi sote bila kujali dini zetu, inajenga na kudumisha upendo, mshikamano na umoja wetu wa kitaifa bila kujali mipaka ya vyama vyetu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More