KIHAMIA:UCHAGUZI SIYO VITA , NI UTARATIBU WA NCHI WA KUPATA VIONGOZI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KIHAMIA:UCHAGUZI SIYO VITA , NI UTARATIBU WA NCHI WA KUPATA VIONGOZI

Na. Vero Ignatus, Liwale,-Lindi

Maandalizi ya uchaguzi mdogo Jimbo Liwale Mkoani Lindi na kata nne Tanzania Bara yamekamikika kwa asilimia 100

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Taifa (NEC) Dkt. Athumani Kihamia kwamba vifaa vimefika wakati hivyo amewataka wananchi wa Liwale watambue kuwa uchaguzi siyo vita bali ni sera ya nchi ya kupata viongozi kwa kuchaguliwa,

"Vifaa vya uchaguzi vimefika kwa wakati, watendaji wa uchaguzi wamepatiwa mafunzo ya kutosha pia ulinzi na usalama umeimarishwa hivyo wananchi msiogope kuja kupiga kura hapo kesho".'' Kwa upande wa kampeni zipo salama hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kurupushani, hakuna malumbano yeyote makubwa ambayo yanaashiria ubunjifu wowote wa Amani''Amesema Kihamia.

Amesema vituo vya kupiga kura vitafunguliwa kesho saa moja asubuhi na vitafungwa majira ya saa kumi jioni 13oktoba 2018, hivyo wananchi wamejitokeze kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi ya Kikatiba ya kupiga kura.Aidha wananchi wametakiwa wakishapiga ku... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More