KIJIJI CHA CHIMBILA B KUSAMBAZIWA MAJI-MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KIJIJI CHA CHIMBILA B KUSAMBAZIWA MAJI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. milioni 250 kwa ajili ya usambazaji wa huduma ya maji safi katika kijiji cha Chimbila ‘B’ kichopo kata ya Mnacho.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Agosti 9, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mnacho wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.Waziri Mkuu amesemaSerikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji, ambapo itahakikisha wananchi wanapata huduma hiyo katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Amesema mbali ya maji kusambazwa kwa wananchi, pia yatasambazwa kwenye taasisi zote za umma zikiwemo shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Mnacho na kuzungumza na wanafunzi, ambapo amesema Serikali inatarajia kujenga mabweni mawili katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kuishi shuleni na kupata fursa nzuri ya kujisomea.Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wanafunzi wa kike shuleni hapo kui... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More