KIKAO CHA WADAU KUHUSU UHAKIKI WA TAKWIMU ZA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI CHAFANA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KIKAO CHA WADAU KUHUSU UHAKIKI WA TAKWIMU ZA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI CHAFANA

Kikao cha Wadau wa Vyama vya Ushirika nchini kimefanyika leo Jumatatu, Aprili 15, 2019 Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili taarifa ya uhakiki wa takwimu za Vyama vya Ushirika na kutoa maazimio juu ya majukumu yanayopaswa kutekelezwa na kila mdau kulingana na matokeo na changamoto zilizobainishwa. Taarifa hii itasaidia katika kuboresha utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika nchini.  
Akifungua kikao hicho, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Bw. Tito Haule  amesisitiza  umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi za Vyama vya Ushirika na amewataka wadau wa ushirika nchini  kutotoa takwimu za Vyama vya Ushirika bila kuwasiliana na mamlaka husika ambayo ni Tume ya Maendeleo ya Maendeleo ya Ushirika.
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ilifanya zoezi la uhakiki wa Takwimu za Vyama vya Ushirika nchini na kupanga SACCOS kwenye madaraja (SACCOS Categorization) mwaka 2018 ili kupata takwimu sahihi za Vyama vya Ushirika. Zoezi hilo lilikamili... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More