KILA LA HERI SIMBA SC….WAPIGENI HAO GOR MAHIA TUPOKEE KOMBE KESHO DAR - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KILA LA HERI SIMBA SC….WAPIGENI HAO GOR MAHIA TUPOKEE KOMBE KESHO DAR

Na Mwandishi Wetu, NAKURU
BINGWA wa michuano ya SportPesa Super Cup 2018 anatarajiwa kupatikana leo kwa mchezo kati ya wenyeji, Gor Mahia na Simba SC ya Dar es Salaam, Tanzania Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya.
Simba SC imefika Fainali baada ya kuzitoa Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys za Kenya pi azote kwa penalti baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90, wakati Gor Mahia ilizichapa 3-0 JKU ya Zanzibar na 2-0 Singida United ya Tanzania.
Baada ya sare ya 0-0 dakika 90, SImba ikaitoa kwa penalti 3-2 Kariobangi Sharks kabla ya kuwatupa nje Kakamega Homeboyz kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 katika Nusu Fainali, kipa wake Aishi Manula ambaye pia ni kipa namba wa Tanzania aking’ara.

Lakini Simba SC itaendelea kuongozwa na Kocha Msaidizi, Mrundi Masoud Juma baada ya kukimbiwa na kocha wake, Mfaransa Pierre Lechantre aliyeanza kazi Januari 18 tu, mwaka huu.
Lechantre na Msaidizi wake aliyekuja naye, Mtunisia Aymen Hbibi Mohammed Alhamisi walikuwa jukwaani wakati Simb... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More